Kikosi cha Simba kimewasili leo jijini kikitokea Sumbawanga ambapo kilikuwa na mchezo wa fainali dhidi ya Namungo FC ambao walipigwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Nelson Mandela.
Wanamsimbazi hao wamerejea na taji la kombe la shirikisho mjini ili kuendeleza shangwe la ubingwa walioutwaa Sumbawanga kwani mashabiki ni ngao yao kubwa na wamekuwa bega kwa bega hivyo inabidi wafurahi kwa pamoja.
Wachezaji wa Simba wamepanda kwenye basi rasmi lililoandaliwa wakiwa na mataji mawili la Ligi Kuu Bara pamoja na Shirikisho wakiwa Kwenye msafara kuelekea Msimbazi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.