Home Makala Madrid Akubali Kipigo Cha Barcelona Fc

Madrid Akubali Kipigo Cha Barcelona Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Real Madrid imekubali kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa klabu ya Fc Barcelona katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini humo (La liga) uliofanyika katika uwanja wa Olimpic Lluis Company nchini humo.

Real Madrid wakiingia katika mchezo huo bila mabeki wake wa kati watatu Antonio Rudiger,Elder Militao na David Alaba  ambao walikua na  kadi za njano pamoja na majeraha iliwashangaza wengi baada ya kupata mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa Kyllian Mbape dakika ya 5 na 14  ambapo  Eric Garcia alifunga kwa kichwa dakika ya 19 huku Lamine Yamal akifunga bao la kusawazisha 32 huku Raphinha alifunga mabao mawili dakika za 34,45 ambapo mpaka mapumziko matokeo yalibaki 4-2.

Kipindi cha pili Barcelona waliendelea kukosa nafasi za wazi ambapo dakika ya 70 Mbape alifunga bao la tatu akipokea pasi ya Vinicious Jr.

banner

Kutokana na ushindi huo sasa Barcelona imefikisha alama 82 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Laliga huku Real Madrid wakiwa na alama 75 katika nafasi ya pili ya msimamo huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 35.

Barcelona wakishinda mchezo unaofuatia dhidi ya Rcd Espanyol siku ya alhamis basi moja kwa moja watakua mabingwa wa La liga msimu huu wa 2024-2025 huku wakiweka rekodi ya kuwafunga mahasimu wao Real Madrid katika michezo yote ya El Classico msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited