Home Makala Majogoro Akana Kutemwa Chipa United

Majogoro Akana Kutemwa Chipa United

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania Baraka Majogoro amekana taarifa za kuwa ameachana na klabu yake ya Chippa United kwa makubaliano ya pande zote mbili zilizozagaa hivi karibuni hapa nchini.

Majogoro (27) ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Afrika Kusini Agosti 2023 hadi 2027 akitokea Klabu ya KMC amesema  kwa sasa bado  ni Mchezaji wa klabu hiyo huku akikanusha vikali taarifa hizo zinazodai kuwa ameachana na klabu hiyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili kuridhiana.

“Ukiniuliza kuhusu kuachana na Chippa napata ugumu kukujibu maana tunavyoongea hivi sasa nipo kazini Chippa, hizo taarifa naziona mtandaoni lakini sijui walioziandika wamezipata wapi pia”,Alisema Majogoro kwa mshangao mkubwa.

banner

“Sijui labda waliondika wanataarifa zaidi juu ya walichoandika, na hata kama kuna kitu kati yangu na Chippa basi hakiwezi kutufikisha kwenye kusitisha mkataba, Mimi sijazungumza na mtu nikathibisha kuachana na Chippa”,Alimalizia kusema Majogoro.

Majogoro ni moja ya mastaa wachache wa Kitanzania wanaocheza soka nchini Afrika ya kusini ambapo mara kadhaa amekua akipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza katika timu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited