Mshambuliaji Heritier Makambo amekubaliana na waajiri wake klabu ya Yanga sc kuvunja mkataba wake ili kupisha maboresho ya kikosi hicho baada ya kushindwa kumpa changamoto staa wa kikosi hiko Fiston Mayele.
Makambo alisajiliwa na Yanga sc misimu mmoja na nusu uliopita ambapo baada ya kutokua na uhakika wa namba kikosini humo ilibidi staa huyo apishe usajjili mwingine mpya wa Kennedy Musonda kutokana na Yanga sc kubanwa na kanuni za usajili wa wachezaji 12 wa kigeni.
Makambo tayari ameshaagwa na klabu hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii imeshachapisha taarifa ya kumuaga staa huyo huku yeye mwenyewe pia amethibitisha kuondoka kwake klabuni hapo ambapo alirejea kwa mara ya pili akitokea klabu ya Horoya Fc ya nchini Guinnea.