Azam Fc imewaongeza muda wa mikataba makocha wake katika benchi la ufundi kwa ajili ya kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21.
Makocha hao ni kocha mkuu, Aristica Cioaba, kocha msaidizi, Bahati Vivier na kocha wa viungo, Costel Birsan, ambapo kila mmoja ameongeza mkataba wa mwaka mmoja.
Azam Fc waliwatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na benchi la ufundi siku ya Jumapili ambalo lilianza kazi kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc na kuibuka na mabao 2-1 katika uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.