Zaidi ya shilingi milioni 100 zimetumika kumshawishi kiungo Mudathir Yahaya kusalia katika klabu ya Yanga sc kwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Mudathir tayari alikua na ofa kutoka klabu za Azam Fc pamoja na Simba sc ambazo zilitaka kumsajili baada ya kuonyesha uwezo mzuri tangu ajiunge na Yanga sc misimu miwili na nusu iliyopita baada ya kushindwana na Azam Fc.
Simba sc walimpa kiungo huyo ofa nono ya mshahara na fungu la kusainia mkataba mpya wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Muzamiru Yassin ambaye kocha Fadlu Davis ameamua kutoendelea naye kutokana na majeraha ya mara kwa mara.
Hata hivyo Pamoja na ofa hizo kiungo huyo anayeweza kucheza kama kiungo mkabaji na mshambuliaji kwa wakati mmoja aliamua kusalia Yanga sc baada ya kufikia muafaka upande wa maslahi akipewa dau nono na mshahara ukipanda mara dufu.
Pia uhakika wa nafasi ya kucheza kikosini humo mara kwa mara kumemshawishi kiungo huyo kusalia klabuni hapo ambapo ameshinda mataji yote ya ndani tangu ajiunge na klabu hiyo.