Kipa mkongwe Aishi Manula yupo mbioni kujiunga na klabu ya Yanga Sc kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya Kimataifa baada ya makubaliano ya pande zote kuanza kufanyika.
Manula anasubiri msimu umalizike ili aondoke msimbazi ambapo ameshakosa nafasi ya kucheza huku pia mkataba wake ukielekea mwishoni na mchezaji mwenyewe hana tena nia ya kuendelea na klabu hiyo.
Mazungumzo hayo mpaka sasa yapo katika hatua za awali ambapo Yanga sc wanamhitaji Manula kuziba nafasi ya Djigui Diarra ambaye amepata ofa nono kutoka vilabu mbalimbali barani Afrika.
Mabosi wa Yanga sc wanaona endapo watafanikiwa kumuuza Diarra basi wataisaini kipa wa klabu ya Singida Black Stars Amos Abasogie pamoja na Manula huku wakiachana pia na kipa Aboubakari Khomeini kutokana na kuwa na makosa mengi uwanjani.
Hata hivyo Pamoja na ofa ya Yanga sc pia kipa huyo yupo mbioni kujiunga na klabu ya Azam Fc ambayo yenyewe inamsaka Manula kutokana na kutokuwa na kipa wa uhakika kati ya Mohamed Mustapha na Zubeiry Foba ambao viwango vyao huwa havitabiriki.