Aliyewahi kuwa mlinda mlango wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Peter Manyika ametangazwa kuwa kocha mpya wa magolikipa wa klabu ya Singida Big Stars (Singida Fountain gates) yenye makazi yake mkoani Singida
Kipa huyo tayari ameanza kazi klabuni hapo na alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la klabu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Simba ambao walipoteza kwa mabao 2-1 siku ya Jumamosi jioni.
Mpaka sasa bado haijafahamika kocha amesaini mkataba wa muda gani lakini tayari amejiunga na miamba hiyo ya soka mkoani humo ili kuwasaidia makipa Benno Kakolanya na wenzake kuhakikisha wanakua na viwango imara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Manyika ni kipa wa zamani wa Yanga sc ambapo pia alikua akijihusisha na kazi ya kuwanoa makipa wachanga kutokana na uzoefu wake katika ngazi ya klabu na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).