Home Makala Mapya Yaibuka Yanga sc Ikiitandika Tp Mazembe

Mapya Yaibuka Yanga sc Ikiitandika Tp Mazembe

by Sports Leo
0 comments

Licha ya kuwazidi ujanja katika usajili wa Kennedy Musonda bado klabu ya Yanga sc imeendelea kuisakama klabu hiyo ikihitaji kumsajili nyota wake Phillip Kinzumbi hasa baada ya mabosi wa klabu hiyo kujiridhisha na ubora wake walipomtazama katika michezo miwili.

Awali katika mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho ambapo Yanga sc iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 Kinzumbi alionyesha kiwango bora na kuwaridhisha mabosi wa timu hiyo yenye maskani yake Jangwani Kariakoo ambapo mpaka kocha Nasredine Nabi naye alivutiwa na uwezo wa winga huyo wa pembeni zaidi.

Katika mchezo wa pili uliofanyika nchini Congo ambapo staa huyo hakucheza lakini mabosi hao kwa kuwatumia baadhi ya watu wanaofahamiana nao nchini humo walipata sifa za kutosha za staa huyo na kuvutiwa kuanza kufanya nae mazungumzo ya kumsajili.

banner

Hata hivyo pia mabosi wa klabu hiyo wakiongozwa na tajiri Ghalib Said Mohamed aliyeambatana na msafara wa timu hiyo pia walifanikiwa kufahamu kuwa mchezaji huyo ana nia ya kuondoka Tp Mazembe ikidaiwa hakuridhika na mkataba mpya aliousaini bila kuuchunguza vizuri huku sasa kazi ikibaki kwa kocha Nabi kama atalipitisha jina hilo katika usajili msimu ujao.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited