Home Makala Mashujaa Chali kwa Jkt Tanzania

Mashujaa Chali kwa Jkt Tanzania

by Sports Leo
0 comments

Pamoja na tambo nyingi sasa Mashujaa Fc ya mkoani Kigoma imekubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Jkt Tanzania katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kambarage mkoani Shinyanga mapema jioni ya leo Oktoba 3.

Bao pekee la mchezo huo limefunga na Edward Songo dakika ya 80 ya mchezo huo uliokua mkali ambapo timu zote mbili zilikua zinashambuliana kwa zamu.

“Kipigo cha kizalendo” maarufu kama double K kama wanavyojitamba Jkt Tanzania kimefanikiwa kuvunja mwiko wa kutofungwa katika mechi tatu walizocheza mashujaa Fc katika ligi kuu mpaka sasa.

banner

Kutokana na matokeo hayo sasa Mashujaa anasaliwa na alama zake 8 huku Jkt Tanzania wakifikisha alama 7 katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Tanzania.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited