Home Makala Mastaa Wakamilika Stars

Mastaa Wakamilika Stars

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) sasa kimekamilika kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Ivory Coast mwakani baada ya awamu ya pili ya mastaa waliokuwa hawajawasili kambini kufanikiwa kuwasili.

Awali kikosi hicho kilisafiri kuelekea nchini Misri utakapopigwa mchezo siku ya Jumapili alfajiri huo kikiwa na mastaa nusu ambapo baadhi ya wachezaji wa Yanga sc walikosekana kikosini kutokana na kuwa na mchezo wa kimataifa dhidi ya klabu ya Us Monastr kutoka nchini Tunisia.

Hatimaye jana mastaa hao waliondoka nchini kuelekea nchini humo wakiwemo Bakari Mwamnyeto,Feisal Salum,Ahmad Abdalah Bacca,Dickson Job,Kibwana Shomari,Metacha Mnata,Mudathir Yahya na Mzamiru Yassin ambaye alikua na matatizo ya kifamilia.

banner

Stars inakabiliwa na mchezo mgumu ugenini dhidi ya Uganda katika kuwania kufuzu fainali hizo ambapo mchezo huo utafanyika nchini Misri kutokana na Uganda kukosa uwanja uliokidhi vigezo vya Caf kutumika katika michuano hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited