Mshambuliaji Fiston Kalala Mayele amefunga mabao matatu katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Zalan Fc katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika mchezo uliokua wa upande mmoja uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Licha ya kuongoza kwa umiliki wa mpira kipindi chote cha mchezo iliwalazimu Yanga sc kusubiri mpaka dakika ya 49 ya kipindi cha pili ili kupata bao la uongozi lililofungwa na Fiston Kalala Mayele ambae aliunganisha kwa kichwa krosi ya Dennis Nkane aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Dickson Ambundo ambaye alianza kipindi cha kwanza.
Dakika tano baadae Feisal Salum alipokea pasi ya Jesus Moloko na kuwachambua mabeki wa Zalan Fc na kuandika bao la pili lililoamsha furaha ya mashabiki wa Yanga sc huku Fiston Mayele akifunga bao la tatu na nne dakika ya 84 na 87 na kuwalazimisha waamuzi kumpa mpira baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja kama ulivyo utaratibu wa siku zote.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Klabu hizo zinatarajiwa kurudiana wiki ijayo ambapo Yanga sc itakua mwenyeji wa mchezo huo ambao utafanyika katika uwanja huo huo baada ya Zalan Fc ya nchini Sudan kusini kutokua na uwanja nchini mwao ambao umeidhinishwa na Caf hivyo kuwalazimu kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wa nyumbani.