Home Makala Mayele Atambulishwa Pyramids

Mayele Atambulishwa Pyramids

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabua ya Pyramids Fc ya nchini Misri imemtambulisha rasmi mshambuliaji Fiston Mayele kutoka klabu ya Yanga sc ambapo mchezaji huyo ataitumikia klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu huku akipewa jezi namba tisa.

Mayele ameondoka Yanga sc baada ya kukaa kwa misimu miwili ambapo kiasi cha takribani bilioni 2.8 kimetumika kukamilisha usajili huo wa staa mkubwa ambaye aliipamba Yanga sc na ligi kuu kwa ujumla.

Mshambuliaji huyo aliyependwa na mashabiki wa Yanga sc hasa kutokana na staili yake ya kutetema wakati akifunga bao alifanikiwa kufunga mabao 16 ya ligi kuu katika msimu wake wa kwanza kisha akafunga mabao 17 katika msimu wake wa pili katika ligi kuu huku akifunga mabao mengine 14 katika michuano ya Caf kuanzia hatua za awali.

banner

Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jamii mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 na ndio Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza na magoli 7.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited