Home Makala Mayele Aweka Rekodi Yanga sc

Mayele Aweka Rekodi Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Fiston Kalala Mayele ameweka rekodi ya kuzifunga timu zote za ligi kuu nchini ispokua klabu za Ruvu Shooting,Tanzania Prisons na Ihefu Fc katika michezo ya ligi kuu nchini tangu asajiliwe na klabu ya Yanga sc akitokea klabu ya As Vita misimu miwili iliyopita.

Mayele amebakisha timu hizo baada ya kufanikiwa kuifunga Mbeya City Fc mabao mawili na kufikisha magoli kumi ya ligi kuu nchini akiwa anaongoza katika mbio za kiatu cha dhahabu huku pia akiweka rekodi ya kufunga jumla ya magoli saba katika mechi tatu za ligi kuu mfululizo.

Baada ya kusuasua katika ufungaji mshambuliaji huyo alianza na Singida Big Stars kwa kuifunga mabao matatu kisha akaifunga Dodoma Jiji Fc mabao mawili na Mbeya City Fc mabao mawili na kukaa kileleni mwa msimamo wa wafungaji huku pia klabu yake ya Yanga sc ikikaa kileleni mwa msimamo kwa alama 32.

banner

Mayele msimu huu ameifungia klabu yake ya Yanga sc mabao 19 katika michezo 17 ya ligi kuu akifunga mabao 10 katika ligi kuu na michuano ya kimataifa akifunga mabao 7 na ngao ya jamii akifunga mabao mawili aliyowafunga Simba sc kitu ambacho pia ni nadra sana kufanywa na washambuliaji wengi wa ligi kuu nchini kwa misimu ya hapa karibuni.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited