Kocha Roberto Oliveira wa Vipers Fc ya Uganda ndiye anatajwa kuwa mrithi wa kocha Nasredine Nabi katika klabu ya Yanga sc siku zijazo baada ya kocha huyo kufanya vizuri na klabu yake na kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika huku akiwapiga vigogo Tp Mazembe na kuwatoa nje ya mashindano hayo makubwa kwa ngazi za klabu Barani Afrika.
Roberto Oliveira ndiye aliyeiongoza Vipers Fc kuifunga Yanga sc katika mchezo wa kilele cha wiki ya mwananchi katika uwanja wa Benjamini Mkapa huku kikosi chake kikionyesha soka safi na kuwazima mastaa wa Yanga sc wakiongozwa na Fiston Kalala Mayele.
Mblazil huyo tayari ameshakubaliana na viongozi wa Yanga sc kuhusu kutua kikosini huku akisisitiza kuwafahamu mastaa wa kikosi hicho pamoja na wapinzani wake ambapo sasa anachosubiri ni uamuzi wa mabosi hao lini atue kikosini humo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mabosi wa Yanga sc inadaiwa walipanga kuitumia mechi ya derby kama daraja endapo wangefungwa lakini kitendo cha Nabi kuibuka na sare kilikwamisha mpango huo.