Home Makala Mbrazil Arejea Simba sc

Mbrazil Arejea Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa klabu ya Simba sc Roberto Oliveira amerejea klabuni kutoka nchini kwao Brazil alipkwenda kwa ajili ya kushughulikia hati yake ya kusafiria sambamba na kusoma kozi ya muda mfupi inayotolewa na shirikisho la soka la nchini hiyo.

Awali Kocha huyo alionekana uwanja wa ndege akisafiri kuelekea nchini kwao na kuzua tafrani miongoni mwa wadau wa soka nchini wakihisi kuwa inawezekana kuwa ametimuliwa klabuni hapo ambapo taarifa rasmi ya klabu ilieleza kuwa ni safari ya muda mfupi akienda kushughulia matatizo binafsi.

Kocha huyo ameiongoza Simba sc katika mechi takribani tatu nne zikiwemo mbili za ligi kuu na mbili za kirafiki zilizofanyika jijini Dubai Falme za Kiarabu alipokwenda na timu hiyo kwa ajili ya kambi ya mafunzo ya muda mfupi kwa mwaliko wa bosi wa klabu hiyo Mo Dewji.

banner

Robertinho kama ilivyo jina lake maarufu atakua na kazi ya ziada kuiongoza klabu hiyo katika mchezo mgumu wa ligi kuu siku ya ijumaa dhidi ya Singida Big Stars utakaofanyika jijini Dar es salaam katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited