Aliyekua kocha wa klabu ya Kagera Sugar Fc Mellis Medo amejiunga na klabu ya Singida Black Stars mara baada ya kuachana na klabu ya Kagera Sugar kutokana na matokeo yasiyoridhisha.
Medo alijunga na klabu hiyo akitokea Mtibwa Sugar lakini sasa klabu hiyo imeamua kuachana nae kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho ambacho sasa kinashika nafasi ya pili kutoka mkiani kikiwa na alama 15 tu katika michezo 21 ya ligi kuu ya Nbc nchini.
Punde tu baada ya kuachana nae tayari klabu ya Singida Black Stars imeamua kumuajiri kocha huyo kama kocha msaidizi huku pia wakimpa kazi ya kulishauri benchi la ufundi la klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Medo raia wa Marekani atashirikiana na makocha David Ouma ambaye ndie kocha mkuu sambamba na Juan Magro na Muhibu Kanu.
Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Singida Black Stars mpaka sasa ipo katika nafasi ya nne ikiwa na alama 38 katika michezo 21 ya ligi kuu nchini.