Home Makala Mgunda Anatosha-Julio

Mgunda Anatosha-Julio

by Sports Leo
0 comments

Aliyekua mchezaji wa zamani wa Simba sc na timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Jamhuri Kihwelo Julio amesema kuwa kocha Juma Mgunda alikua anatosha katika nafasi ya kocha mkuu wa klabu hiyo aliyopewa kocha wa sasa Roberto Oliveira.

Julio amesema hayo mapema hivi leo alipokua katika mahojiani na kituo cha Radio ya Wasafi Fm ambapo alisisitiza kuwa Simba sc ilifanya makosa kumshusha cheo kocha huyo na kumpa ukocha msaidizi.

“Mgunda alistahili kubaki kuwa kocha mkuu wa Simba,mtu anafanya vizuri na wachezaji wanamkubali unamtoa kwanini?Lakini kwa interest za watu wakaamua kumtoa”Alisema kocha huyo aliyewahi kuvinoa vilabu mbalimbali hapa nchini.

banner

Mgunda alikua kocha wa Coastal Union ambapo aliteuliwa kuwa kocha wa muda wa klabu ya Simba sc akisaidiwa na Seleman Matola kisha baadae akaletwa kocha mpya Zoran Maki ambaye baada ya kutimuliwa Mgunda aliiongoza tena Simba sc katika mechi kadhaa kwa mafanikio makubwa mpaka pale alipokuja Mbrazil Roberto Oliveira akitokea Vipers Fc na kushika jukumu la ukocha mkuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited