Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Albert Chalamila ameongoza makapuni mbalimbali katika kuisapoti klabu ya Yanga sc kuelekea mchezo wa fainali ya kwanza dhidi ya Usm Algers kwa kununua tiketi za mashabiki ili kusaidia kuujaza uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo tiketi hizo zitagawiwa bure.
“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameunga mkono hamasa ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kununua tiketi 𝟭𝟬𝟬𝟬 za mchezo wetu wa fainali”Ilisomeka taarifa iliyotolewa na Yanga sc kupitia mitandao rasmi ya kijamii ya klabu hiyo.
Pia mdhamini mkuu wa Ligi Kuu benki ya NBC imeipongeza Yanga kuingia fainali ya Komne la Shirikish na kuahidi kutoa tiketi 1000 kwa ajili ya mashabiki wa Yanga kuelekea mchezo wa fainali Mei 28,2023 dhidi ya USM Algiers uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.
Huku pia Baraza la michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya michezo Tanzania wametoa jumla ya tiketi 10,000 kwa ajili ya kuzigawa kwa washabiki watakaokwenda kuangalia mechi ya kwanza ya fainali kombe la shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na USM Alger itakayochezwa uwanja wa Mkapa Jumapili hii Mei 28,2023.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Benki ya CRDB pia imetoa jumla ya tiketi elfu tano za mashabiki kupitia kwa mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela ili wananchi wajae uwanjani kuongeza hamasa kuelekea mchezo huo.