Home Makala Mkude Ampeleka Mo Dewji Mahakamani

Mkude Ampeleka Mo Dewji Mahakamani

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Jonas Mkude amefungua shauri katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam akiishtaki kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) kutokana na kutumia picha zake katika mitandao ya X na Instagram bila kuwa na makubaliano yeyote.

Katika shauri hilo mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Simba sc anadai fidia ya Sh 1 bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na X (zamani Twitter) bila idhini yake.

Mkude amefungua kesi ya madai 192 ya mwaka 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip dhidi ya kampuni hiyo akiidai fidia hiyo Kwa kuvunja haki yake ya msingi na kutimia picha zake kutangaza biashara za kampuni hiyo bila makubaliano ya msingi.

banner

Mkude amejiunga na Yanga sc msimu huu akitokea Simba sc aliyotumikia kwa misimu 12 tangu alipojiunga na timu ya wakubwa ya klabu hiyo akitokea timu ya vijana.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited