Home Makala Mo Akutana na Mastaa Simba sc

Mo Akutana na Mastaa Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Mwenyekiti wa zamani wa bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Simba sc Bilionea Mohamed Dewji amekutana na wachezaji na viongozi wa klabu hiyo katika kikao cha pamoja baada kurejea nchini akitokea nje alipokua katika shughuli zake za kibiashara.

Mo ambaye ni Rais wa heshima wa klabu hiyo amekutana na wachezaji wa klabu hiyo kujadili mambo mbalimbali huku kubwa ikielezwa ni mwenendo wa timu hiyo kwenye ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa ambayo inatarajiwa kuanza siku ya jumapili ambapo klabu hiyo itavaana na timu ya Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast.

Simba sc itaanza kampeni yake katika michuano ya kombe la shirikisho ikiwavaa Asec Mimosa kisha baada ya siku sita itawavaa USGN na baadae kucheza na Rs Berkane Februari 27.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited