Winga kiberenge Jesus Moloko ataukosa mchezo wa ufunguzi wa michuano mifupi ya ngao ya jamii dhidi ya Azam Fc baada ya kuwa na adhabu ya kukosa michezo miwili kutokana na kadi nyekundu aliyoipata msimu uliopita katika mchezo dhidi ya Mbeya City Fc.
Moloko alipata kadi hiyo baada ya kugombana na Nassoro Machezo katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja huo wa kumbukumbu ya Sokoine jijini humo licha ya Yanga sc kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Tayari mchezaji ameshatumikia adhabu hiyo kwa kukosa michezo miwili ukiwemo huo dhidi ya Tanzania Prisons wa kufunga pazia la ligi kuu na ule wa dhidi ya Azam Fc wa fainali ya kombe la shirikisho nchini ambapo Yanga sc waliibuka na ushindi wa 1-0 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.