Home Makala Morrison Akubali Yaishe

Morrison Akubali Yaishe

by Sports Leo
0 comments

Winga hatari Benard Morrison amekubali yaishe baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha kwa klabu hiyo kutokana na kosa la utovu wa nidhamu uliosababishwa asimamishwe na klabu hiyo.

Morrison baada ya kusimamishwa akituhumiwa kutoroka kambini mara kwa mara pamoja na kuchelewa kurudi hasa anapopewa mapumziko baada ya mechi ambapo kutokana na makosa hayo aliondolewa kikosini huku akitakiwa kuandika barua ya kuomba radhi kwa Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Babrah Gonzalez.

Awali ilidaiwa kuwa mchezaji huyo aligoma kuandika barua hiyo lakini hivi leo imethibitishwa kuwa amendika barua hiyo na kuiwasilisha kama alivyoelekezwa kwa mujibu wa Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba sc Ahmed Ally.

banner

Morrison amekua na kawaida ya utovu wa nidhamu tangu alipowasili hapa nchini ambapo alijiunga na klabu ya Yanga sc kwa mkataba wa miezi sita kisha kujiunga na Simba sc kwa mkataba wa miaka miwili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited