Home Makala Morrison Asepa Yanga sc,Kutua Singida FG

Morrison Asepa Yanga sc,Kutua Singida FG

by Sports Leo
0 comments

Winga machaxhari Benard Morrison yupo mbioni kujiunga na klabu ya Singida Fountain Gate Fc inayoshiriki ligi kuu nchini baada ya kuachana na klabu ya Yanga sc alipodumu kwa msimu mmoja pekee licha ya kusajili kwa gharama kubwa ya mshahara.

Mabosi wa Yanga sc walikua na matumaini makubwa na Morrison kuwa atafanya maajabu baada ya kumrejesha kutokea Simba sc lakini staa huyo alishindwa kutumika katika mechi nyingi msimu huu kutokana na sababu mbalimbali ikwemo majeraha na utovu wa nidhamu.

Yanga sc baada ya kuachana na staa huyo tayari klabu ya Singida Fountain Gate ipo mbioni kumsajili ili kumtumia hasa katika michuano ya kimataifa ambapo watashiriki katika kombe la shirikisho kuanzia msimu ujao baada ya kumaliza ligi katika nafasi ya nne.

banner

Kikwazo kikubwa katika kukamilisha dili hilo ni kiwango cha mshahara wa staa huyo ambapo alipokua Yanga sc alikua akipokea zaidi ya shilingi milioni 20 za kitanzania na endapo atakubali kupunguza basi dili hilo linaweza kutangazwa muda wowote kuanzia sasa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited