Home Makala Morrison Azua Taharuki,Asaini Simba

Morrison Azua Taharuki,Asaini Simba

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Benard Morrison ametambulishwa rasmi leo ndani ya kikosi cha Simba ukiwa ni usajili wa kwanza kwa ajili ya msimu wa 2020/2021.

Thamani ya dau lake linatajwa kuwa ni zaidi ya milioni 150 ambayo amepewa ili kujiunga na klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili.
Morrison amekuwa na mvutano mkubwa na mabosi wake kwenye suala la mkataba ambapo mchezaji alisema kuwa ana dili la miezi sita huku uongozi ukisema kuwa amesaini dili la miaka miwili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited