Home Soka Mshery Asaini Mitatu Yanga Sc

Mshery Asaini Mitatu Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imemfunga kipa AbouTwalib Msheri kusalia klabuni hapo kwa miaka mitatu zaidi baada ya mkataba wake wa awali kumalizika na kuzima tetesi za kuhitajika na klabu ya Azam Fc pamoja na klabu zingine za ligi kuu nchini.

Msheri alijiunga na Yanga sc akitokea Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili lakini sasa ataendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2027 sambamba na Djigui Diarra ambaye nae amesaini mkataba wa muda mrefu kusalia klabuni hapo.

Awali ilisemekana kipa huyo alikua na mpango wa kuondoka klabuni hapo baada ya kupata ofa kutoka klabu ya Azam Fc ambayo ilimhitaji kwenda kusaidiana na kipa Mohamed Mustafa katika michuano ya ligi kuu na kombe la klabu bingwa barani Afrika.

banner

Msheri ana kazi nzito ya kufanya ili kuvunja utawala wa Diarra ambaye ni kipenzi cha wanayanga kutokana na kuwaokoa katika nyakati ngumu mchezoni ambapo mara kadhaa ameikoa timu hasa katika mechi dhidi ya Medeama Fc akidaka penati ya Jonathan Sowah na katika mchezo wa fainali dhidi ya Azam Fc kombe la Shirikisho ambapo aliokoa penati ya Lusajo Mwaikenda na kuipa ubingwa wa kombe hilo klabu hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited