Home Makala Msuva Ashinda Kesi Fifa

Msuva Ashinda Kesi Fifa

by Sports Leo
0 comments

Winga wa Taifa Stars Simon Msuva ameshinda kesi dhidi ya klabu ya Wydad Casablanca juu ya madai ya mishahara yake na fedha za usajili ambazo hakulipwa kipindi anaichezea klabu hiyo hivyo kuamua kuishtaki katika shirikisho la soka duniani (Fifa).

Msuva licha ya kuishtaki klabu hiyo alimua kuachana nayo na kuamua kurudi nyumbani ambapo alikaa akisubiri uamuzi wa Fifa kuhusu hatma yake ambapo aliruhusiwa kucheza mpira ili kulinda kipaji chake kwa mujibu wa kanuni ambapo alijiunga na klabu ya Al-Qadsiah ya nchini Saudi Arabia huku akisubiri maamuzi kutoka mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo (Cas) baada ya klabu hiyo kukata rufaa kufuatia uamuzi wa Fifa wa kumpa ushindi Msuva na kuamuru klabu hiyo imlipe zaidi ya bilioni moja za kitanzania.

Sasa muda si mrefu mahakama hiyo imetoa maamuzi kuhusu kesi hiyo ambapo Wydad wameamliwa kumlipa  mchezaji wao wa zamani Msuva kiasi cha dola za Kimarekani 720,000 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni moja na nusu za Kitanzania au kufungiwa kufanya uhamisho wa wachezaji.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited