Site icon Sports Leo

Mturo Apewa Fainali FA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza majina sita ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa fainali kombe la Azam (ASFC) utakaofanyika Jumapili August 2,2020 mkoani Sumbawanga Uwanja wa Nelson Mandela kati ya Simba Sc na Namungo Fc.

Abubakari Mturo kutoka Mtwara ni moja ya muamuzi atakayekuwepo katika mchezo huo baada ya kutoka kwenye kifungo cha miezi mitatu tangu Februari baada ya kushindwa kumudu mchezo kati ya Yanga Sc dhidi ya Lipuli Fc.

Waamuzi wengine wakiwa ni Abdallah Mwinyimkuu kutoka Singida,Ahmed Arajiga kutoka Manyara,Ramadhani kayoko kutoka Dar-es-salaam,Abdullaziz Ally kutoka Arusha na Hamdan Said kutoka Mtwara.

Exit mobile version