AFC Leopard imemuongezea mkataba mpya wa miaka miwili beki,Washington Munene ambaye alikuwa nyota wa zamani wa Nairobi Stima.
Munene aliingia kambini mwa Leopard mwanzoni mwa msimu wa 2019/2020 baada ya kuagana na Wazito Fc kwa mkopo.
Beki huyo anakamilisha idadi ya wachezaji watatu baada ya kiungo Collins Sichenje na raia wa Uganda,Benjamin Ochan kurefusha mkataba wake kambini humo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Leopards kwa sasa wanashiriki mazungumzo na fowadi Elvis Rupia kuhusu uwezekano wa kutia saini mkataba mpya baada ya kandarasi yake ya awali kumalizika Aprili 2020.