Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kumsajili na kumtambulisha mshambuliaji Kennedy Musonda aliomsajili kutokea Power Dynamo ya Zambia kwa mkataba wa miaka miwili kuja kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo iliyochini ya Fiston Kalala Mayele.
Musonda ambaye anaongoza katika chati ya wafungaji bora ya ligi kuu ya soka nchini Zambia amejiunga na Yanga sc baada ya klabu hiyo kuvunja mkataba wake na Power Dynamo huku pia ikimpatia donge nono yeye binafsi na kufanikiwa kuwazima Tp Mazembe waliokua katika nafasi nzuri ya kumsajili baada ya kukubalina nae baadhi ya mambo.
Inasemekana katika dili hilo Yanga sc imetumia takribani kiasi kinachikadiriwa kufikia Milioni mia tano ikiwa ni malipo ya kuvunja Mkataba katika timu yake pamoja na dau la usajili la Musonda ambaye pia atapokea takribani shilingi milioni 11 za kitanzania kama mshahara wa kila mwezi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc imemsajili mshambuliaji huyo ikiwa ni matakwa ya kocha Nasreddine Nabi aliyetaka aletewe mshambuliaji mmoja,kiungo na beki ili kupata kikosi imara cha kupambana katika kombe la shirikisho barani Afrika kuanzia mwezi ujao.