Mastaa wa ligi kuu nchini Tanzania Kennedy Musonda na Clotous Chama wameitwa katika kikosi cha Chipolopolo chini ya kocha Avram Grant kwa ajili ya michizo ya awali ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2023).
Kocha Avram Grant alifika nchini wiki zilizopita kwa ajili ya kuwatazama mastaa hao wakizitumikia klabu zao za Simba sc na Yanga sc katika michuano ya kimataifa kwa lengo la kujiridhisha zaidi kuhusu viwango vya na hatimae ameamua kuwaita katika kikosi hicho.
Chama tayari ni mzoefu wa kuitwa katika timu ya Taifa tofauti na Musonda ambapo kikosi hicho kinakabiliwa na mchezo mkali dhidi ya Lesotho kuwania nafasi ya kufuzu michuano hiyo itakayofanyika nchini Ivory Coast.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.