Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuinasa saini ya winga wa klabu ya Power Dynamos Joshua Mutale kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kumalizana na timu yake ya Power Dynamos ya nchini Zambia ambapo tayari klabu hiyo imemtambulisha rasmi.
Winga huyo anatua klabuni hapo ikiwa usajili wa pili kutangazwa msimu huu baada ya awali klabu hiyo kutangaza kumsajili beki Lameck Lawi kutoka Coastal Union Fc ya jijini Tanga kwa mkataba wa miaka mitatu huku ikiwa imewaongezea mikataba mastaa kama Kibu Dennis,Mzamiru Yassin na Israel Mwenda ambao watadumu kikosini hadi mwaka 2026.
Simba sc imeamua kufanya maboresho makubwa ya kikosi chake ili kufanya vizuri katika ligi na michuano ya kimataifa kuanzia msimu ujao baada ya kuwa na misimu mibovu takribani mitatu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Joshua anatajwa kama winga mwenye kasi huku akiwa na uwezo wa kucheza nafasi ya mshambuliaji wa pili ama winga wa kulia ama kushoto ambapo msimu uliomalika amecheza jumla ya michezo 26 akiwa na klabu ya Power Dynamos ya nchini kwa Zambia akifunga mabao 5 na kutoa assisti 4.