Huu ndio muonekano mpya wa beki wa Simba, Pascal Wawa baada ya kukaa kipindi cha mpito ndani ili kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona akiwa nje ya kambi ya Simba.
Inasemekana wachezaji wengi walihofia hata kwenda saluni kutolewa nywele kwa kuhofia maambukizi ya Virusi vya Corona.
Shughuli zote za kimichezo zimeruhusiwa kuanza rasmi Juni Mosi na Raisi wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania,Dr.John Pombe Magufuli huku masuala ya ligi kuhudhuliwa na mashabiki akiliacha chini ya wizara ya afya itoe maamuzi ili kulinda afya za wananchi.