Kiungo wa klabu ya Simba Sc Mzamiru Yassin hatokuwa tena sehemu ya kikosi cha Simba Sc kuelekea msimu ujao wa ligi kuu ya Nbc baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa mwezi juni 2025.
Mkataba wake na waajiri wake hao umekwisha na hakuna mazungumzo mapya kuhusu kuongeza mkataba mpya ndani ya mitaa ya msimbazi.
Kiungo huyo hayupo katika mipango ya kocha wa Simba Sc Fadlu Davies na badala take kocha huyo amewaambia mabosi wa Simba sc kuhakikisha wanaingia sokoni kusaka vyuma vipya kuelekea msimu ujao.
Kuondoka kwa Mzamiru kunahitimisha miaka takribani tisa ya staa huyo kukaa klabuni hapo akisajiliwa msimu wa 2016/2017 akitokea katika klabu ya Mtibwa Sugar.
Mzamiru miaka ya hivi karibuni alikua na wakati mgumu klabuni hapo kupata nafasi katika kikosi cha kwanza miaka ya hivi karibuni kutokana na eneo la kiungo la klabu hiyo kujaa mastaa wa kimataifa.