Home Makala Mzungu Avunja Mkataba Simba sc

Mzungu Avunja Mkataba Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Dejan Georgijević ameweka bayana kuondoka klabuni hapo kwa madai ya Uongozi wa klabu hiyo kutomtimizia baadhi ya mahitaji ya kimkataba na hivyo kuuvunja mkataba huo kutokana na kutomiza baadhi ya vipengele muhimu katika makubaliano ya kimkataba aliousaini mapema wakati anajiunga na klabu hiyo msimu huu.

Dejan alibainisha hayo kupitia katika mtandao wake wa Instagram ambapo alindika “Ninathibitisha kwamba mkataba wangu wa ajira umevunjika kutokana na kutotimizwa kwa mambo muhimu na klabu asanteni mashabiki kwa sapoti na upendo mlionipa”Ulisomeka ujumbe huo ambapo dakika chache ulisambaa na kuzua gumzo miongoni mwa wadau wa soka nchini.

Hata hivyo kuondoka kwa mchezaji huyo klabuni hapo kulitarajiwa na mashabiki wengi baada ya mshambuliaji huyo kushindwa kuwashawishi walimu wa klabu hiyo akiwemo kocha Zoran Maki ambaye alikua akimtumia kama mbadala wa Habib Kiyombo na huku mwalimu Juma Mgunda naye akishindwa kumpa nafasi mbele ya Moses Phiri ambaye huwa anaanza mara kwa mara.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited