Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga Sc Nasredine Nabi amevutiwa na mshambulia wa Al Ittihad ya Libya na sasa klabu yake ya Kaizer Chiefs imefungua mazungumzo rasmi na mshambuliaji huyo ili kumsajili kuunda kikosi kikali cha msimu ujao wa ligi kuu ya soka ya Mtn nchini Afrika ya Kusini.
Kaizer Chiefs inafahamu kuwa mchezaji huyo dau lake linatajwa kufikia kiasi cha €900k sawa na Bilioni 2.78 za Kitanzania na wanaangalia uwezekano wa kufanya mazungumzo kupunguza dau hilo ili wamsajili moja kwa moja kuongeza nguvu kikosi hicho ambapo msimu huu kimechukua kombe moja baada ya kukaa miaka kumi bila kombe lolote.
Simba SC kutoka Tanzania ilikuwa inahusishwa kuhitaji huduma yake msimu uliomalizika ila makubaliano hayakwenda sawa upande wa maslahi ambapo walishindwa kukubaliana na dau kubwa la mshambuliaji huyo pamoja na mshahara wake wa mwezi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Nabi amekubaliana na mabosi wa klabu hiyo kufanya usajili wa mastaa mbalimbali ili kuongeza makali katika kikosi hicho na tayari ameshawaona mastaa kama Feisal Salum,Jean Charles Ahou na Mohamed Damaro Camara ambapo mpaka sasa anaangalia upatikanaji wao sokoni.