Klabu ya Yanga sc ipo mbioni kuachana na kocha wake pamoja na kuvunja benchi la ufundi lililochini ya kocha Nasreddine Mohamed Nabi na Cedrick Kaze baada ya timu kuwa na mwenendo mbaya hasa wa masuala ya kinidhamu kwa wachezaji wa klabu hiyo.
Inasemekana kwamba wawili hao hawaeleni kwa muda mrefu wao kwa wao huku pia wakishindwa kudhibiti nidhamu ya mastaa wao kikosini kwa muda hali inayomlazimu bosi mkubwa wa klabu hiyo kuingilia kati mara kwa mara ili kuweka mazingira sawa ya kambi pamoja na mazoezi.
Nabi ambaye ameiongoza Yanga sc kutofungwa katika michezo 43 ya ndani anakabiliwa na presha kubwa klabuni hapo ikiwemo suala ya kufanya vibaya katika michuano ya kimataifa baada ya kutolewa na Al Hilal Fc na kushindwa kuiingiza klabu hiyo katika hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika ambapo sasa wanalazimika kucheza mchezo wa Play-off na Club Africains kutoka nchini Tunisia ili kufuzu makundi ya kombe la shirikisho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mipango ya mabosi wa Yanga sc ni kumuajiri kocha wa klabu ya Vipers Fc ya Uganda Mbrazil Roberto Oliveira kuja kuchukua nafasi ya Nabi huku Kaze akipelekwa kusimamia timu ya vijana na timu ya wanawake ya klabu hiyo jambo ambalo amekua na uzoefu nalo.