Home Makala Nabi Kutua Kaizer Chiefs

Nabi Kutua Kaizer Chiefs

by Dennis Msotwa
0 comments

Taarifa kutoka nchini Afrika ya kusini zinarripoti kuwa klabu ya Kaizer Chiefs imefikia makubaliano na kocha Nasredine Nabi kujiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Yanga sc kwa mafanikio makubwa msimu huu.

Nabi inasemekana tayari yupo mbioni kuondoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo huku akitarajia kulipwa takribani kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia ambapo ameweka sharti la kuja na wasaidizi wake akiwemo kocha wa viungo na mtaalamu wa kuwasoma wapinzani.

Mapema hivi leo kocha huyo amekutana na viongozi wa Yanga sc kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya ambapo inasemekana wameshindwa kukubaliana haswa katika masuala ya kimaslahi ikizingatiwa kuwa kocha huyo ana ofa hiyo nono kutoka Kaizer.

banner

Wakala wa kocha huyo ambaye ni mwanae Hedi Nabi amesema kuwa bado haijajulikana kama ataondoka ama la mpaka amalize mazungumzo na Yanga sc kwanza ndio atajua kipi kinafuata.

“Siwezi kusema anaondoka wala anabaki kwasasa,b baba yangu ni mtu anayeheshimu viongozi mashabiki na hata wachezaji wake lakini kitu ambacho kitakwenda kutoa picha halisi ya baadaye ni pale atakapokutana na uongozi wa klabu yake,” alisema Hedi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited