Home Makala Nani Baba Lao?

Nani Baba Lao?

by Dennis Msotwa
0 comments

Hatimaye baada ya dakika 90 za mechi baina ya watani wa jadi Simba na Yanga zimemalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar-es-salaam.

Alikuwa Meddie Kagere aliyeitanguliza Simba kwa penati dakika ya 43 baada ya kufanyiwa faulo na Kelvin Yondani na mwamuzi Jonesia Rukyaa kuizawadia Simba penati iliyoipa bao la kuongoza.

Kipindi cha pili dakika ya 47 Deo Kanda alifunga bao la pili baada ya uzembe wa mabeki wa Yanga kushindwa kulinda lango na mpira uliopigwa na Shomari Kapombe kumkuta Kagere aliyemtulizia mfungaji.

banner

Dakika ya 49 Balama Mapinduzi alipiga shuti kali lililomshinda kipa Aishi Manula na kuipa Yanga goli la kwanza lililowarejesha mchezoni na dakika nne baadae wakapata goli la kusawazisha kupitia kwa Mohamed Hussein aliyejifunga kwa kichwa.

Licha ya kosakosa za hapa na pale dakika 90 za mchezo zilimalizika kwa sare na hivyo Simba kubaki kileleni wakiwa na pointi 35 huku yanga wakipanda mpaka nafasi ya 3 wakiwa na pointi 25.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited