Mabao mawili ya Neymar dakika ya 6 na 90+2 yalitosha kuipa ushindi wa 3-0 timu ya Paris St.German dhidi ya Manchester United katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya.
Neymar alifunga mabao hayo kutokana na uzembe wa mabeki wa Man United huku pia Marquinhos akifunga dakika ya 69 baada ya Marcus Rashford kuisawazishia united dakika ya 31.
Sasa Man United wana kazi ya kufanya ili kufuzu hatua ya 16 bora watakapokua ugenini kuivaa Lb Leipzig huku wakihitaji alama moja kufuzu kupitia kundi hilo la H.