Azam FC imemuongezea mkataba mshambuliaji , Obrey Chirwa huku uongozi wa timu hiyo umeonekana hauna mpango wa kumuongezea mkataba nyota wake, Donald Ngoma.
Uongozi wa Azam FC Unadai kuwa Ngoma amekuwa hana mwendelezo mzuri ndani ya klabu hiyo kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara hali inayofanya ashindwe kuonyesha kiwango bora na kutoa mchango wake kwenye timu hiyo.