Home Makala Nigeria Majanga Tupu

Nigeria Majanga Tupu

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya Taifa ya Nigeria imeshindwa kufuzu kuelekea katika michuano ya kombe la dunia baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Ghana katika mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Nigeria katika uwanja wa Taifa wa Abuja.

Thomas Partey kiungo wa klabu ya Arsenal aliwatanguliza wageni kwa bao la uongozi dakika ya 10 bao ambalo halikudumu baada ya Nigeria kupata bao la penati likifungwa na William Troost-Ekong na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika 90 za mchezo na Ghana kufanikiwa kufuzu kwenda nchini Qatar katika michuano mikubwa kwa ngazi ya timu.

Dakika tisini za mchezo zilipokamilika Ghana hawakuwa na muda wa kufurahia ushindi baada ya fujo kutawala uwanjani hapo ambapo mashabiki wa Nigeria walianza kufanya fujo kwa kuwashambulia wachezaji wa Ghana na mashabiki wao ambapo inaripotiwa kwamba daktari raia wa Zambia Joseph Kabungo ambae jana alikuwa ofisa wa CAF katika mchezo huo amefariki dunia.

banner

Ghana sasa inaungana na timu za Cameroon,Senegal,Tunisia na Morroco kuiwakilisha Afrika katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za timu za Taifa huku ikiwa ni michuano inayofuatiliwa zaidi duniani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited