Beki wa klabu ya Yanga sc Abdalah Shaibu ‘Ninja’ ameuomba uongozi wa klabu ya Yanga sc kumruhusu kwenda kwa mkopo katika klabu ya Geita Gold Sc ambayo imeonyesha nia ya kumsajili kwa mkopo wa msimu mzima.
Ninja ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga sc baada ya kocha Nabi kumhitaji kikosini licha ya uongozi wa klabu hiyo kuonyesha nia ya kutomuongezea mkataba ambao ulikua umeisha na tayari alikua amesharejea nyumbani kwao Zanzibar kujipanga kutafuta timu nyingine.
Geita Gold Sc ambayo itashiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la shirikisho ipo katika harakati za kujenga kikosi chake ili kupata uhakika wa kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi za vilabu barani Afrika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.