Home Makala Nkane Nje Wiki Sita

Nkane Nje Wiki Sita

by Sports Leo
0 comments

Winga wa klabu ya Yanga sc Dennis Nkane atakua nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita akiuguza majeraha ya nyonga aliyoyapata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam wiki chache zilizopita na klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Nkane aliingia kipindi cha pili ambapo hakumaliza mchezo huo baada ya kugongana na mchezaji wa Coastal Union na kutolewa nje kwa matibabu ikiwa zimebaki dakika takribani kumi mchezo kumalizika na kusababisha Yanga sc kucheza pungufu kwa muda huo baada ya kuwa wamemaliza nafasi zote za kufanya mabadiliko.

Taarifa iliyotolewa na Timu ya Madaktari wa klabu ya Yanga sc inaonyesha kuwa Nkane atahitaji wiki nne za matibabu huku ikiwa wiki mbili za mazoezi madogomadogo ili kujiweka fiti kabla ya kujiunga rasmi na kikosi hicho kumalizia mechi zilizobaki za ligi kuu na michuano ya kimataifa.

banner

“Vipimo vimeonyesha alivunjika mfupa unaosababisha nyonga kukunja ndiomana alipata maumivu makali sana na tayari tumeshaanza taratibu ya matibabu na atakuwa na vipimo viwili kabla ya kurejea moja kwa moja uwanjani. “Atakaa nje kwa wiki nne halfu wiki mbili za mwisho ataanza mazoezi mepesi ambayo tutakuwa tunamfuatilia kujua maendeleo yake.” alisema Dokta Moses Etutu daktari wa Yanga sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited