Klabu ya soka ya Yanga imetoa taarifa rasmi ya kuachana na Afisa mhamasishaji wa timu hiyo Antonio Nugaz ambaye mkataba wake wa miaka miwili umemalizika.
Klabu ya Yanga imeamua kutomuongezea Nugaz mkataba baada ya kumaliza mkataba wake wa awali aliousaini miaka miwili iliyopita akiwa kama Afisa mhamsishaji wa klau hiyo yenye makao makuu mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo.
Nugaz atakumbushwa kwa mchango wake mkubwa kuwahamasisha mashabiki wa Yanga kwa kauli zake kama ‘wape salam’ iliyojizolea umaarufu nchini,hata hivyo kuondoka kwake kunatajwa kutokana na Yanga kumuajiri aliyekuwa msemaji wa Simba Haji Manara.
Â
Â