Home Makala Nzengeli,Gamondi Wachukua Tuzo

Nzengeli,Gamondi Wachukua Tuzo

by Sports Leo
0 comments

Mchezaji wa klabu ya Yanga sc Maxi Nzengeli Mpia pamoja na kocha Miguel Gamondi wamefanikiwa kuchukua tuzo ya kocha bora na mchezaji bora kwa mwezi wa nane huku meneja wa uwanja wa Manungu mkoani Morogoro unaomilikiwa na klabu ya Mtibwa Sugar Godfrey Komba akifanikiwa kuchukua tuzo ya meneja bora wa uwanja.

Kwa mujibu wa utaratibu bodi ya ligi kuu nchini huchagua mchezaji,kocha na meneja bora wa uwanja kila mwezi ambapo kwa mwezi uliopita mwezi wa nane Max amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo akiwazidi Stephane Aziz Ki wa Yanga na Jean Baleke wa Simba sc ambapo Maxi amekua na mchango mkubwa zaidi kuliko hao.

Pia kocha Gamondi amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo akiwazidi Roberto Oliveira wa Simba sc na Hemed Morroco wa Geita Gold Sports Club ambapo ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KMC na Jkt Tanzania vilimnyanyua kocha huyo.

banner

Tuzo hizo hutolewa kila mwezi kwa wachezaji,makocha na mameneja wa uwanja waliofanya vizuri ambapo bodi ya ligi imeunda kamati maalumu ya kuchambua takwimu na kutangaza mshindi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited