Inadaiwa mambo ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba sc Emmanuel Okwi katika klabu ya Al Ittihad nchini Misri baada ya kucheza mechi 14 ndani ya timu yake hiyo ametupia mabao mawili.
Kiwango duni na nafasi finyu ndio vinavyotajwa kuwa vinaweza kumrudisha staa huyo nchini huku klabu ya Simba sc ikitajwa kuwania saini yake japo mipango inafanyika kimyakimya.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema:” Kwa sasa kocha ametoa mapendekezo yake ya mchezaji wa kusajiliwa na kuachwa, hatuwezi kuweka wazi siri za klabu muda ukifika kila kitu kitajulikana,”.