Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Pacome Zouzoua amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni hapo baada ya mkataba wake wa awali kumalizika.
Pacome ametambulishwa na klabu hiyo kama mchezaji anayeendelea kukipiga klabu hapo na kuzima tetesi za kukaribia kujiunga na klabu nyingine hapa nchini.
Sasa mashabiki wa Yanga sc watakua wanapata usingizi kutokana na kutambulishwa kwa mchezaji huyo kama mchezaji anayeendelea kusalia klabuni hapo huku mastaa kama Cletous Chama na Khalid Aucho wakiondoka.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tayari klabu hiyo imetangaza kuachana na Cletous Chama pamoja na Jonas Mkude sambamba Khalid Aucho,Stephen Aziz Ki ambaye amepata dili katika klabu ya Wydad Athletic ya nchini Morocco.