Inter Milan imeingia kwenye bato la timu nne zinazopambana kumng’oa Paulo Pogba huko Manchester United kwenye usajili wa msimu ujao.
Nyota huyo Mfaransa anaonekana kuwa mguu ndani nje Man United hasa baada ya mwenyewe kukiri kutaka kwenda kutafuta changamoto mpya kwingineko.
Kocha wa Real Madrid,Zinedine Zidane kwa muda mrefu amekuwa akimtaka kiungo huyo anayeshikilia rekodi ya kusajiliwa kwa pesa nyingi ligi kuu England lakini kuna mpango pia wa kiungo huyo kurudi Juventus mahali ambapo alishatamba kwa miaka 4 kuanzia 2012/2016.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Paris Saint-Germain pia wanataka kuinasa saini ya nyota huyo ili kucheza ndani ya Ufaransa ikiwa ni baada ya kuwauza Neymar ndani ya Barcelona.