Home Makala Prince Wa Azam Azidi Kung’ara

Prince Wa Azam Azidi Kung’ara

by Sports Leo
0 comments

Prince Dube mwenye hasira ya kuchukua kiatu cha dhahabu ndani ya msimu huu mpya wa ligi kuu 2020/2021 ambacho kwa sasa Meddie Kagere anakishikilia ,anazidi kujiwekea akiba ya mabao ndani Azam Fc akiwa amefunga jumla ya mabao matano huku mpinzani wake Kagere akiwa na mabao manne pekee ndani ya Simba Sc.

Azam Fc inayonolewa na kocha mkuu,Arstica Ciaoba imezidi kushika kinara ligi kuu bara baada ya kuwatungua mabao 4-2 Kagera Sugar kwenye mchezo wa raundi ya tano ya ligi kuu uliochezwa jana uwanja wa Chamazi majira ya saa1:00 usiku na kufikisha pointi 15 huku simba wakiwa nafasi ya pili na alama 13.

Dube alitupia mabao mawili katika mchezo huo ambapo bao la kwanza alifunga dakika ya 6 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huku lile jingine alilitupia dakika ya 88 ya kipindi cha pili cha mchezo kabla ya kipenga cha kumaliza mchezo kupigwa.

banner

Dakika ya 48 Obrey Chirwa wa Azam Fc hakuwa nyuma kupachika bao la pili baada ya kutoka mapumziko huku Richard Djodi akitupia bao la tatu dakika ya 52.

Kipa wa Azam Fc,David Kissu kwa mara ya kwanza jana kuruhusu mabao mawili katika lango lake kutoka kwa David Luhende wa Kagera Sugar dakika ya 34 na jingine dakika ya 50 kupitia Yusuph Mhilu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited